"Ataufanya wema wako ung'ae kama mwanga, na uadilifu wako kama jua la adhuhuri." (Zaburi 37:6) Jua linaangaza mchana, na mwezi huangaza usiku. Mwezi hauwezi kuangaza mchana, wala jua kuangaza usiku. Mungu kaumba jua na mwezi kusudi viangaze mahali pake na kwa wakati wake ulioamriwa. Kama vile mwezi huangazavyo usiku na jua liangazavyo mchana; angaza mahali pale ambapo Mungu amekuweka uingazie dunia kwa mwangaza wake.
Tunapoishi kwa haki, wema, na uaminifu, maisha yetu huanza kung’aa kama mapambazuko ya alfajiri. Hatuhitaji kujilinganisha na wengine; tunahitaji tu kuangaza mahali ambapo Mungu ametuweka. Matendo yetu yanapoakisi wema wake, watu huona mwanga ndani yetu na kumtukuza Mungu. “Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.” (Mathayo 5:16)