Skip to Content

YESU NIJALIE MOYO WA SALA

6 Februari 2026 na
YESU NIJALIE MOYO WA SALA
Sr. Violet Kwanungu LSOF

"Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi wake." (Luka 11:1)

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa uchaji na imani thabiti..

Nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa utulivu na usikivu.

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa moyo na kwa matumaini.

Nijalie moyo wa sala nipate kusali kwa unyenyekevu na upendo.

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali wakati wa furaha na wakati wa shida na mahangaiko.

Nijalie moyo wa sala nipate kusali kila wakati na mahali popote.

Ee Yesu, nijalie moyo wa sala nipate kusali ningali hai na saa ya kufa.

Amina.

katika Blogu yetu
YESU NIJALIE MOYO WA SALA
Sr. Violet Kwanungu LSOF 6 Februari 2026
Shiriki posti hii
Lebo
Maktaba