Skip to Content

SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU

17 Aprili 2026 na
SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU
Sr. Violet Kwanungu LSOF

Mtakatifu Mikaeli Malaika Mkuu, utulinde katika vita, uwe kinga yetu katika maovu na maoteo ya shetani. Mungu amtiishee tunaomba sana, nawe Mkuu wa Majeshi ya Mbinguni kwa nguvu ya Mungu uwaangushe motoni shetani na pepo wabaya wengine wote wanaozunguka duniani, ili kuzipoteza roho za watu. Amina

“Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo, vaeni silaha za Mungu ili siku ile itakapofika mweze kuyapinga mashambulizi ya adui; na mkiisha kupigana mpaka mwisho, mtakuwa bado imara.” (Waefeso 6:11-13)

“Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwepo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 8:38-39)

“Basi, kaeni tayari. Ukweli na uwe kama ukanda kiunoni mwenu, uadilifu uwe kama vazi la kujikinga kifuani, na hamu ya kutangaza Habari Njema ya amani iwe kama viatu miguuni mwenu. Zaidi ya hayo yote, imani iwe kama ngao mikononi mwenu, iwawezeshe kuizima mishale ya moto ya yule mwovu. Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu. Salini daima, mkiomba msaada wa Mungu. Salini kila wakati kwa nguvu ya Roho. Kesheni bila kuchoka mkisali kwa ajili ya watu wote wa Mungu.” (Waefeso 6:14-18)

katika Blogu yetu
SALA KWA MTAKATIFU MIKAELI MALAIKA MKUU
Sr. Violet Kwanungu LSOF 17 Aprili 2026
Shiriki posti hii
Lebo
Maktaba