Furaha ya kweli kwa mwanadamu haiko katika wingi wa vitu alivyonavyo, bali katika kumjua na kumpenda Mungu, ambaye ndiye mwenye vitu vyote. Furaha ya mwanadamu hukamilika katika Mungu, ambaye ana upendo wa kweli. "Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu." (Warumi 5:8)
Furaha ya mwanadamu hutimilika katika Mungu, ambaye anatusamehe dhambi zetu." Basi tumsifu Mungu kwa sababu ya neema yake tukufu ambayo ametujalia katika Mwanaye mpenzi. Maana kwa damu yake Kristo sisi tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa. Ndivyo ulivyo ukuu wa neema yake aliyotukirimia bila kipimo kwa hekima na ujuzi wake wote." (Waefeso 1: 6-8)
Furaha ya mwanadamu hutimilika katika Mungu, ambaye anaponya magonjwa yetu."Yesu alitembea kote Galilaya, akifundisha Habari Njema kuhusu Ufalme, na kuponya watu waliokuwa na aina zote za magonjwa na maradhi." (Mathayo 5: 23) Furaha ya mwanadamu hutimilika katika Mungu, ambaye anatuliza dhoruba katika maisha yetu. Furaha ya mwanadamu hutimilika katika Mungu, ambaye anatusaidia katika nyakati za shida. Furaha ya mwanadamu hutimilika katika Mungu, ambaye anatuimarisha katika majaribu yote."Anasema, 'Nyamaza, na ujue ya kuwa mimi ni Mungu; nitakuzwa kati ya mataifa, nitakuzwa katika dunia." (Zaburi 46:10)
Furaha ya mwanadamu hutimilika katika kutimiza mapenzi ya Mungu. Furaha ya mwanadamu hukamilika tuwapo katika muunganiko na Mungu. Furaha ya mwanadamu itakamilika tunapoungana na Mungu mbinguni. "Utanijulisha njia ya uzima, mbele za uso wako ziko furaha tele; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele." (Zaburi 16:11)