"Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu; asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia." (Zaburi 5:3)
Asubuhi ni kibali chako cha kuanza siku mpya, Mungu katuzawadia siku mpya ya kuishi tena duniani. Anza siku yako kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, usisahau kumuomba akuongoze na kukulinda. Usiruhusu asubuhi yako kuharibiwa, maana utapoteza amani yako na uwezo wako wa kufanya kazi kwa ufanisi.
Usigombane na mtu yeyote asubuhi, la sivyo utapoteza amani yako ya ndani na kushindwa kutekeleza majukumu yako vizuri. Amani yako ya moyo na roho ndio uchangamfu wako na furaha yako, itunze amani yako.
Linda siku yako ili ikulinde, na usiruhusu amani yako ipotee, ili siku yako iweze kubarikiwa na Mungu. Linda siku yako ili ikulinde, ili mwishoni mwa siku hii mpya uwe na furaha na umshukuru Mungu Mwenyezi.